
Mbinu za Siri Wafanyabiashara Wakubwa Wanazitumia Kupata Utajiri!
Wadau wa BongoBox, Karibuni!
Wadau wa BB, habari za siku? Poleni na pilika pilika za maisha, najua mitaa imewaka, wengi wanahaha huku na kule kutafuta mkate wa kila siku. Lakini si wote wanahaha – wapo wale waliotoboa, wanadunda bila stress, huku wengine wakibaki wakiwatazama tu kwa mshangao. Swali ni moja: Wanatumia mbinu gani? Mchezo upo wapi?
Leo tunavunja ukimya. Tunakwenda kuchimba mambo ambayo wengi hawayaelewi, lakini yanatumiwa na wachache kuujaza mfuko bila vumbi. Huu si uzi wa kawaida. Soma hadi mwisho, utashangaa ni kwa vipi unahangaika bila sababu.
1. Kuelewa Mfumo: Pesa Hazipatikani kwa Bahati, Zinachorwa
Wenye nacho wanajua kitu kimoja: Fedha si kitu cha kubahatisha, ni kitu cha kuandaliwa.
Watu wa kawaida wanategemea mshahara, lakini wenye nacho wanajua kuwa pesa haitafutwi kwa jasho peke yake, inatengenezwa kwa akili. Kila kitu tunachoona – bei ya unga, mafuta, viwanja, hadi gharama ya maziwa – hakina bahati humo, kuna watu wanazichora. Wale wanaojua kuusoma mchezo wanajiweka kwenye nafasi sahihi. Huwezi kuwa na pesa ikiwa unacheza mchezo wa waliopangiwa kupoteza.
Sasa swali: Mchezo wenyewe ukoje?
2. Mchezo wa Mtaji: Pesa Inakua Kwa Mfumo, Si Kwa Kuhifadhi
Wenye nacho hawashikilii pesa kwa hofu kama tunavyofanya sisi.
Mtu wa kawaida akipata hela, jambo la kwanza ni kufikiria jinsi ya kuitumia.
Lakini mwenye nacho akipata hela, jambo la kwanza ni kufikiria jinsi ya kuiotesha.
Ukweli ni huu: Pesa haikai benki kwa matajiri. Benki ni sehemu ya maskini kuhifadhi, lakini matajiri wanaitumia kwa mchezo mwingine. Wanaweka pesa kwenye mfumo wa riba, wawekezaji wa hisa, miradi isiyoonekana, au hata biashara zinazoonekana ziko hoi lakini zinachapisha pesa kimyakimya.
Mfano hai: Unajua kuna watu wanakopa benki, wanazungusha pesa kwenye biashara nyingine, wanatengeneza faida, na kulipa mkopo bila kutumia hela yao? Hii si bahati, ni mfumo.
3. Biashara za Siri: Maji Marefu Hayana Giza
Unaweza kuona mtu ana duka dogo la vifaa vya ujenzi(Hardware), lakini unashangaa anavyoishi maisha ya kifalme. Siri ni kwamba duka ni pazia tu, mzigo mkubwa uko nyuma ya pazia. Wengine wana miradi ya ardhi, wana mkono kwenye tender za serikali, au wanaingiza mzigo wa bidhaa fulani ambayo huioni mtaani ila imezagaa kwenye maghala ya matajiri.
Mfano mwingine ni wenye biashara za hoteli au baa. Unadhani pesa wanayoingiza ni kutoka kwenye vyakula na vinywaji tu? La hasha! Wengine wanaingiza hela kupitia mfumo wa watu wanaokodisha vyumba kwa mikataba ya kimya kimya, wengine wanaingiza kupitia huduma ambazo hazipo kwenye menu rasmi ya biashara.
Somo? Kama huwezi kuona biashara yenyewe, basi biashara ni wewe!
4. Mkakati wa Kujua Watu Sahihi: Mafanikio ni Connection, Sio Elimu Pekee
Watu wengi wanaamini kuwa elimu ndiyo kila kitu. Ukweli mchungu ni kwamba elimu peke yake haitoshi. Wenye nacho wanafahamu kuwa kujua mtu sahihi ni bora kuliko kuwa na vyeti vya degree 10.
Ndio maana utakuta mtu hana hata diploma lakini anasonga mbele kwenye miradi mikubwa.
Watu wana connection, wanajua nani wa kumpigia simu ili dili lipite.
Wanajua wapi pa kuwekeza, nani wa kushirikiana naye, na nani wa kumkwepa.
Unataka kutoboa? Jifunze lugha ya matajiri: NETWORKING.
5. Mchezo wa Kodi: Pesa Haipotei, Inabadilisha Njia
Hebu jiulize, kwanini matajiri wengi wana kampuni badala ya biashara binafsi? Jibu ni kodi.
Kampuni inaweza kupata misamaha ya kodi, lakini mtu binafsi hana huo uhuru.
Kampuni inaweza kutumia gharama zake kupunguza kiasi cha kodi inayopaswa kulipa.
Matajiri wengi wanajua jinsi ya kuhamisha pesa kwa kutumia sheria zilizopo.
Ndiyo maana unakuta kampuni inafanya biashara Tanzania lakini inalipa kodi nchi nyingine. Wana mfumo wa “tax haven” ambapo pesa zao zinapitia njia ambazo watu wa kawaida hawaelewi.
Somo hapa? Usiangukie kwenye mtego wa kulipa kila senti bila kujua mbinu za kihasibu.
6. Kutengeneza Brand: Jina Lako Lina Thamani Kubwa Kuliko Pesa
Huwezi kujua nguvu ya jina hadi litakapotumiwa kuzalisha pesa bila hata kufanya kazi. Tajiri si mtu mwenye hela nyingi tu, ni mtu mwenye jina lenye thamani.
Mfano hai: Unaweza kuwa na biashara ya kawaida tu, lakini ukiweza kujenga jina la kuaminika, wateja watakufuata wenyewe. Matajiri wanatumia ujanja huu kutengeneza mali hata bila kuwa na mtaji mkubwa.
Wanatumia jina lao kupata mikopo.
Wanatumia jina lao kupata wawekezaji.
Wanatumia jina lao hata kufanya biashara bila kutumia hela zao.
Somo? Jenga jina lako, liwe na thamani zaidi ya pesa.
7. Kuficha Mali: Matajiri Hawana Pesa, Wanamiliki Vitu
Huwezi kuona tajiri ana akaunti iliyojaa mamilioni benki. Hapana! Wenye nacho wanajua kuwa pesa ikikaa benki inaibiwa na mfumuko wa bei. Badala yake, wanahifadhi mali kwenye:
-Ardhi
-Hisa
-Dhahabu
-Mali zisizoonekana moja kwa moja kama “intellectual property”
Ukitaka kuelewa mchezo huu, jiulize: Mbona matajiri wakubwa hawavai dhahabu nyingi lakini wana ukwasi wa ajabu? Jibu ni kwamba utajiri wao hauonekani moja kwa moja, lakini upo kwenye mifumo isiyoshikika.
Mwisho kabisa: Ukifungua Macho, Utajua Mchezo
Wadau wa BB, huu ni mwanga wa kwanza tu. Mchezo upo, lakini si kwa kila mtu. Wanaofanikiwa wanajua siri ya pesa haiko kwenye bahati, bali kwenye kuelewa mfumo.
Unataka kujua zaidi? Tupia comments zako, huenda tukachimba zaidi!
Kama kuna kitu hakijakaa sawa kwako, uliza.
Kama una siri nyingine unayojua, weka hapa, wacha tujifunze!
Ukweli ni huu: Pesa haionekani kwa macho, lakini huwezi kuikosa ukiujua mchezo.
3 Comments
Optimist21
ahsante sanaaa
March 3, 2025New Guest
Duuh.. leo ndo nimeelew naxhuk xn
June 15, 2025
lapulgadre
Duh nawasikitikia tu ambazo hawana hii app